HAWA NI MSHABIKI WA SIMBA NA YANGA JIJINI ARUSHA WAKICHUANA KATIKA NANI MTANI JEMBE. SASA NI ZAMU YA RUVUMA NA NGOMA ITAPIGWA MJINI SONGEA |
Na Mwandishi Wetu
Mashabiki
wa Simba na Yanga mjini Songea watamenyana vikali katika michezo mbalimbali
kupitia bonanza maalum la Nani Mtani Jembe lililoandaliwa na Bia ya Kilimanjaro
Premium Lager litakalofanyika uwanja wa Maji Maji mjini Songea Jumapili wikendi
hii.
Mratibu
wa Bonanza hilo Amadeus Kalumuna, amesema kuwa michezo mbalimbali ikiwemo soka
bonanza la wachezaji saba kila upande, kuvuta kamba, na pia mpira wa mezani
maarufu kama fussball itapamba bonanza hilo.
Burudani mbalimbali pia zitapamba
bonanza hilo zikiwemo burudani ya muziki kutoka bendi ya Mastaa wa Kusini,
kikundi cha sanaa cha Umoja Star au maarufu kama “Manyoka”, wacheza show wa
Chicharito Group pamoja na wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya wa
mkoani Ruvuma.
Kalumuna
pia amesema kuwa vilevile kuwa michezo mbalimbali ya kujifurahisha kama vile
kufukuza kuku wa kienyeji, kukimbia na gunia na kupiga penati ukiwa umefungwa
kitambaa usoni itapamba bonanza hilo ambalo ni la kwanza kufanyika katika mkoa
wa Ruvuma kupitia Nani Mtani Jembe. Kampeni hii ya aina yake inatoa fursa ya
kipekee kwa mashabiki hao kujumuika pamoja na kuburudika na vile vile imeongeza
chachu ya ushindani na utani wa jadi kati ya mashabiki hao huku ikiwapa fursa
ya kipekee kuonyesha mapenzi kwa timu zao.
Bonanza
hilo linalotarajiwa kuanza saa tatu asubuhi ni mwendelezo wa kampeni ya Nani
Mtani Jembe ambayo ilizinduliwa Oktoba 2 na inafanyika nchi nzima
ikiwashirikisha mashabiki wa timu kongwe za Simba na Yanga. Kupitia kampeni
hiyo, Kilimanjaro Premium Lager inayozidhamini timu za Simba ya Yanga imetenga
kiasi cha shilingi milioni 100 na kisha kuzigawanya kwa timu hizo ambapo kila
timu inazo shilingi milioni 50 ambazo zinashindaniwa na mashabiki wao.
Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe alisema kuwa mashabikiwa Simba na Yanga
wanatakiwa kushindana kwa kushiriki kwenye kampeni hiyo ili kuhakikisha kuwa
timu mojawapo inapata fedha nyingi zaidi ya timu nyingine.
Akielezea
namna ya kushiriki, Kavishe alisema kuwa mpaka kila timu imetengewa shilingi
milioni 50 na kuwa mshiriki wa shindano hilo la Nani Mtani Jembe ambaye ni
shabiki wa Simba au Yanga anachotakiwa kufanya ni kununua bia ya Kilimanjaro
Premium Lager ambayo kwenye kizibo chake kuna namba ya kushiriki.
Alisema
baada ya shabiki kununua bia ya Kilimanjaro na kuona namba ya kwenye kizibo,
anachotakiwa kufanya ni kuchukua simu yake ya kiganjani na kuandika ujumbe
mfupi wa maneno akianza na jina la timu anayoshabikia kisha anaandika namba
iliyo kwenye kizibo na kuituma kwenye namba 15440.
Alisema
baada ya shabiki kutuma namba hiyo, atakuwa amepunguza shilingi 1,000 kutoka
kwa timu pinzani yaani ikiwa shabiki aliyetuma ujumbe huo ni wa Simba atakuwa
amefanikiwa kupunguza shilingi 1,000 kutoka kwenye fungu la Yanga na ikiwa
shabiki ni wa Yanga pia atakuwa amepunguza shilingi 1,000 kutoka kwa Simba.
Kwa
mujibu wa Kavishe matokeo ya uwiano wa fedha zinavyopungua kutoka Simba au
Yanga yatangazwa kila siku hadi siku ya mwisho wa shindano hilo Desemba 14,
mwaka huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment