Michuano
ya Kombe la Chalenji inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika
Mashariki na Kati (Cecafa) inafanyika Kenya kuanzia Novemba 27 hadi Desemba 12
mwaka huu.
Nchi
wanachama ambazo zinataka kushiriki zinatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kwa
Sekretarieti ya Cefaca kabla ya Oktoba 20 mwaka huu.
Wanachama wa Cecafa ni
Burundi, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudan, Sudan
Kusini, Tanzania, Uganda na Zanzibar.
Michuano
hiyo itatanguliwa na Mkutano Mkuu wa CECAFA utakaofanyika Novemba 26 mwaka huu
ambao pamoja na mambo mengine utakuwa na ajenda ya uchaguzi. Uchaguzi huo ni
kwa ajili ya kujaza nafasi nne za wajumbe wa Kamati ya Utendaji.
Wajumbe
wanaomaliza muda wao ni Sahilu Gebremarian wa Ethiopia ambaye pia ni Makamu
Mwenyekiti wa CECAFA, Abdigaani Saed Arab (Somalia), Tariq Atta (Sudan) na
Raoul Gisanura (Rwanda).
Majina
ya wagombea yanatakiwa kuwa yamewasilishwa katika Sekretarieti ya CECAFA kabla
ya Oktoba 20 mwaka huu, na yakiwa yamethibitishwa na vyama vyao vya mpira wa
miguu.
0 COMMENTS:
Post a Comment