PAPIC |
Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limewasilisha rasmi suala la madai ya
aliyekuwa Kocha wa Yanga, Kostadin Papic dhidi ya klabu hiyo katika Kamati ya
Hadhi ya Wachezaji.
FIFA
imesema imepeleka rasmi suala hilo katika kamati yake hiyo baada ya kupokea
vielelezo vya Papic anayedai kuidai Yanga dola 10,000 za Marekani pamoja na
vile vya Yanga inayodai kumlipa kocha huyo fedha zote alizokuwa akiidai klabu
hiyo.
Kwa
taratibu za FIFA, hivi sasa haitapokea vielelezo vingine kutoka pande hizo
mbili, na badala yake Kamati hiyo inayoongozwa na Theo Zwanziger kutoka
Ujerumani itafanya uamuzi na kuziarifu pande husika. Zwanziger kitaaluma ni
mwanasheria.
Papic
aliyeinoa Yanga kwa vipindi viwili tofauti aliwasilisha malalamiko yake FIFA
akidai hadi mkataba wake unamalizika klabu hiyo ilikuwa haijamlipa dola 10,000
za Marekani.
0 COMMENTS:
Post a Comment