Kamati
ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imefanya marekebisho ya
ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ili kupisha mechi ya mchujo ya Kombe la
Dunia kati ya Tanzania na Msumbiji.
Mechi
hiyo ya kwanza ya raundi ya kwanza kwa mashindano ya wanawake wenye umri chini
ya miaka 20 itachezwa Jumamosi (Oktoba 26 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam kuanzia saa 10 jioni.
U20
tayari imehamishia kambi yake hosteli ya Msimbazi Center, Dar es Salaam kutoka
JKT Ruvu mkoani Pwani tangu wiki iliyopita kujiandaa kwa mechi hiyo. Fainali za
Kombe la Dunia kwa U20 wanawake zitafanyika mwakani nchini Canada.
Marekebisho
ya ratiba ya VPL yamegusa raundi zote tatu zilizobaki kukamilisha mzunguko wa
kwanza. Kutokana na marekebisho hayo mechi za raundi ya 11 zitakuwa ifuatavyo;
Oktoba 28 mwaka huu ni Coastal Union vs Mtibwa Sugar, Oljoro JKT vs Ashanti
United, Ruvu Shooting vs Kagera Sugar na Simba vs Azam. Oktoba 29 mwaka huu ni
Tanzania Prisons vs Mbeya City, Yanga vs Mgambo Shooting na Rhino Rangers vs
JKT Ruvu.
Raundi
ya 12 ni kama ifuatavyo; Oktoba 31 mwaka huu ni Simba vs Kagera Sugar, Novemba
1 mwaka huu ni JKT Ruvu vs Yanga. Novemba 2 mwaka huu ni Mgambo Shooting vs
Coastal Union, Tanzania Prisons vs Oljoro JKT, Azam vs Ruvu Shooting, Mtibwa
Sugar vs Rhino Rangers na Mbeya City vs Ashanti United.
Raundi
ya 13 ni kama ifuatavyo; Novemba 6 mwaka huu ni JKT Ruvu vs Coastal Union,
Ashanti United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs
Tanzania Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar. Novemba 7 mwaka huu ni Azam
vs Mbeya City.
Mechi
za kufunga raundi ya 10 zitachezwa keshokutwa (Oktoba 23 mwaka huu) kama ratiba
inayoonesha. Mechi hizo ni kati ya Coastal Union vs Simba, Tanzania Prisons vs
Kagera Sugar na Yanga vs Rhino Rangers.
0 COMMENTS:
Post a Comment