October 31, 2013


Mshambuliaji wa Simba, Amissi Tambwe amesema atacheza katika mechi ya leo dhidi ya Kagera Sugar kama makocha Abdallah Kibadeni na Jamhuri Kihwelo wataona anastahili kufanya hivyo.


Simba inashuka dimbani leo katika mechi ngumu ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar.

Tambwe ambaye anaongoza kwa kufunga mabao na sasa akiwa sawa na Hamis Kiiza wa Yanga, amesema amepania kucheza mechi hiyo lakini ni uamuzi wa walimu hao.

“Walimu ndiyo wataamua, maana nimekuwa nikisumbuliwa na maumivu na siku moja ya juzi nilikaa nje bila ya kufanya mazoezi.

“Ndiyo maana nasema walimu wataamua kuhusiana na hilo, mimi niko tayari kucheza kwa kuwa nataka kushirikiana na wenzangu kuisaidia timu yetu,” alisema Tambwe.


Tokea alipofunga bao la nane wiki tatu zilizopita, Tambwe hajafunga tena na hivi karibuni Kiiza amemfikia na kuwa sawa naye kwa mabao nane kila mmoja na ndiyo wanaoongoza listi ya wafungaji bora.

1 COMMENTS:

  1. Kiukweli huwa siridhiki na unavyoripoti taarifa zako. Uko-bias sana, huwezi na kwa hili huwezi kudumu wana huwezi kuacha legacy kwenye Tasnia ya Habari; kwa hali hii huwezi compite even within East Africa . Try be professional...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic