October 11, 2013





Mshambuliaji wa Simba, Amissi Tambwe amesema anajisikia yuko vizuri baada ya kushindwa kufanya mazoezi siku chache zilizopita.
Tambwe raia wa Burundi amesema alifanya mazoezi jana na atafanya leo.


“Niko vizuri, unajua nilisikia mwili unakosa nguvu tu, lakini sasa niko safi kabisa naomba Mungu anisaidie Jumamosi ifike vizuri,” alisema.

Simba kesho inaivaa Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
 
Simba itafanya mazoezi mara moja leo kwenye uwanja wa hoteli ya Bamba Beach, Kigamboni jijini Dar ambako kikosi hicho kimeweka kambi.

Tambwe amekuwa tegemeo la Simba katika ufungaji mabao na tayari amepachika manane na ndiye kinara katika Ligi Kuu ya Vodacom ambayo bado ni mbichi kabisa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic