October 12, 2013



Kutokana na matokeo ya jana ya michuano ya awali kuwania kucheza Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil, timu nyingine tatu zimepata nafasi huku nyingine zikitakiwa kusubiri.


Ujerumani, Switzerland na Ubeligiji ndiyo zimefanikiwa kufuzu huku England pamoja na kuichapa Montenegro italazimika kusubiri.

Mabingwa wa dunia Hispania wao walishinda mabao 2-1 dhidi ya Belarus inayoshika mkia, nayo imekaribia na italazimika kujihakikishia kama imefuzu katika mechi itakayofuata.

Ubelgiji iliifunga Croatia kwao kwa mabao 2-1, Ujerumani ikaichapa Ireland 3-0 na Swiss ikaimaliza Albania 2-1.


Cristiano Ronaldo na Ureno yake analazimika mchezo wa mtoano kwa kuwa walilazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Israel.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic