October 12, 2013

PRISONS

 Kocha wa Prisons ya Mbeya, Jumanne Chale ametaka mwamuzi wa mchezo wa leo dhidi ya Simba kuchezesha fair.

Chale amesema kikosi chake kinajiamini kuwa kitafanya vizuri katika mechi ya leo na wana nafasi kubwa ya kuifunga Simba.


“Mechi ya leo itakuwa ngumu, kamwe hatuwezi kusema tunaibeza Simba. Lakini tunataka mwamuzi achezeshe haki.

“Kama tutafungwa na tunaona hakuna tatizo kwa waamuzi, basi hatuwezi kuwa na sababu ya kulalamika,” alisema Chale.

Mara nyingi, mechi kati ya Simba na Prisons imekuwa na ushindani mkali.

Timu hizo zinakutaka kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic