October 10, 2013




Watoto na vijana wabunifu katika eneo la Chamazi jijini Dar es Salaam walifanikiwa kushuhudia bure mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Azam FC dhidi ya Mgambo Shooting.



Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar, vijana hao walipanda juu ya miti tena katika matawi yasiyo imara ya mnazi na kushuhudia kwa dakika 90.


Watu hao walionyesha wana uzoefu mkubwa na miti hiyo kwani walienjoy vilivyo huku wakishangilia kama kawaida sawa na watu waliokuwa kwenye majukwaa.

Azam ilishinda kwa mabao 2-0 katika mechi hiyo na kuchupa hadi nafasi ya pili ya Ligi Kuu Bara, nyuma ya vinara Simba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic