October 10, 2013




Muigizaji maarufu raia wa Marekani, Hayden Panettiere ndiye mwanamke aliyeshikilia moyo wa bingwa wa duniani wa uzito wa juu katika masumbwi, Wladimir Klitschko.

Hivi karibuni Klitschko amekubali yaishe baada ya kumvisha Hayden pete ya uchumba iliyoelezwa ni ya almasi.




Hayden ni raia wa Marekani na amekuwa akiingiza filamu na tamthilia mbalimbali ikiwemo ile ya Heroes.

Wawili hao wamekuwa pamoja kuanzia mwaka 2009, mara kadhaa waliachana na kurudiana, lakini safari hii wameamua kufanya kweli.



Wawili hao wamekuwa kivutio zaidi kwa kuwa Klitschko ana urefu wa futi 6 na inchi 6 na anamzidi mwanadada huyo zaidi ya futi 1 na inchi kadhaa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic