November 30, 2013


Muda mchache ujao kipa Yaw Berko raia wa Ghana atasaini mkataba wa miezi sita kuichezea Simba katika mzunguko wa pili.


Kipa huyo mzoefu ametua nchini asubuhi hii badala ya jana jioni kama ilivyokuwa imelezwa hapo awali.

Hata hivyo, Berko hakutaka kuzungumza masuala mengi zaidi badala yake amesisitiza aachiwe hadi hapo atakapokutana na uongozi wa Simba.

“Nitazungumza zaidi hapo baadaye baada ya kuzungumza na viongozi na kujua ni I hasa tunakwenda kufanya na mwisho wake ni nini,” alisema.
Simba imekuwa ikihaha kumsaka kipa mzoefu baada ya uongozi kufikiak uamuzi wa kuachana na Mganda Abel Dhaira ambaye kiwango chake kimeporomoka.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic