November 12, 2013


Na Mwandishi Wetu, Nairobi
Rais mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameitwa ili kukaa na kujadiliana na shirikisho la hapa KFF ili kuboresha nguvu ya maendeleo katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Rais wa Shirikisho la Soka Kenya (KFF), Sam Nyamweya amesema anaamini Malinzi ni kati ya watakaochangia kasi ya maendeleo ya soka katika ukanda huu.

Akizungumza nyumbani kwake jijini hapa, Nyamweya alisema  Malinzi ni kati ya watu anaoamini watanga vizuri kwa kuwa ni mchapakazi.

“Tayari nimeandaa utaratibu ikiwezekana nikutane na Malinzi, tujadili masuala kadhaa kwa ajili ya maendeleo pamoja kama nchi za Afrika Mashariki na baadaye nitafanya hivyo kwa Uganda, Rwanda na Burundi.

“Inawezekana kabisa kufanya kitu vizuri mkiwa pamoja, kila upande utafanya juhudi kuendelea sehemu husika na baada ya hapo tunachangia kama ukanda wetu.

“Itakuwa kazi ngumu sana kuendelea na kushindana na Kaskazini na Magharibi mwa Afrika kama tutaendelea kutengana na kila mmoja anafanya mambo yake tu,” alisema Nyamweya.

“Hata kama kuna tatizo na tunaona Caf wanatusumbua au kuna kitu kinatukandamiza, inaweza kufikia wakati tukapiga kelele pamoja na kupinga.”


Alisema kuhusiana na mwaliko wa Malinzi, atawasiliana naye na kuangalia ligi atakuwa na nafasi naye pia lini ana nafasi, halafu atalifanyia kazi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic