November 1, 2013


Hatimaye Halmashauri ya Jiji la Mwanza imetuma dola 118,000 (Sh milioni 190) kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kwa ajili ya kuweka nyasi bandia na ujenzi wa majukwaa kwenye Uwanja wa Nyamagana.


Fedha hizo zimetumwa Fifa kupitia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuchangia mradi huo ambao gharama zake zinafikia dola 618,000 (Sh 990m), tayari Fifa ilishatoa dola 500,000 (Sh 800m).


Meya wa Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula amesema fedha hizo zilitolewa mwanzoni mwa mwezi huu.

Fifa ilitaka Mwanza ichangie kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kuanza uwekaji wa nyasi hizo bandia katika uwanja huo mkongwe.

Wakati fulani serikali ilitaka kujenga hoteli kubwa katika eneo la uwanja huo lakini ikapata upinzani mkubwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic