November 22, 2013



 
KIPA NTALLA AKIWA NA KIKOSI CHA KAGERA MSIMU ULIOPITA
Kocha Msaidizi wa Kagera Sugar, Mrage Kabange amesema walimshauri aliyekuwa kipa wao, Andrew Ntalla, asiende Simba kwa kuwa kiwango chake kilikuwa bado lakini akakaidi na sasa hawana mpango naye hata kama atahitaji kurejea klabuni hapo.


Kabange amesema awali kipa huyo waliyemtoa timu ya Magereza iliyokuwa ikishiriki Ligi Daraja la Tatu Sumbawanga walimshauri na kumtaka asubiri kwanza kwa kuwa kiwango chake kilikuwa hakijafikia kuichezea Simba lakini akabisha.

“Sisi tulimshauri kama wazazi wake lakini hakutuelewa basi tukamuacha tu, si unajua walimwengu wanasema mtoto akililia wembe mpe nasi tukamuacha,” alisema Kabange.

Aliongeza hawawezi kumrudisha tena Kagera kwa kuwa wao tayari wana makipa watatu ambao ni Hannington Kalyesabula, Agatoni Antony na mwingine ambaye wamempandisha kutoka U 20.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic