November 22, 2013





Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 23 watakaoshiriki katika Michuano ya Kombe la Chalenji inayofanyika nchini Kenya kuanzia Novemba 27, mwaka huu.


Kili Stars iliyotwaa kombe hilo mara ya mwisho mwaka 2010 chini ya Kocha Jan Poulsen na ambayo imepangwa Kundi B katika michuano ya mwaka huu, itacheza mechi yake ya kwanza Novemba 28 mwaka dhidi ya Zambia kwenye Uwanja wa Machakos.

Wachezaji waliojumuishwa kikosini: makipa ni Deogratius Munishi (Yanga), Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya) na Aishi Manula (Azam), ambapo kipa wa Yanga, Ally Mustapha ‘Barthez’ hajajumuishwa kikosini.

Mabeki ni Erasto Nyoni, Himid Mao, Ismail Gambo, Said Moradi (wote Azam), Kelvin Yondani (Yanga) na Michael Pius (Ruvu Shooting).

Viungo ni Amri Kiemba, Haruna Chanongo na Ramadhan Singano (wote Simba), Athuman Idd, Frank Domayo (wote Yanga), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting) na Salum Abubakar (Azam).

Washambuliaji ni Elias Maguli (Ruvu Shooting), Faridi Musa, Joseph Kimwaga (wote Azam), Juma Luizio (Mtibwa Sugar), Mrisho Ngassa (Yanga), Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta (wote TP Mazembe, DRC).

Kili Stars inatarajiwa kuondoka Jumatatu (Novemba 25) kwenda Nairobi kwa ajili ya michuano hiyo itakayoanza Novemba 27 na kumalizika Desemba 13, 2013.

Wakati huohuo, mechi ya kirafiki kati ya Taifa Stars dhidi ya Zimbabwe iliyochezwa Jumanne wiki hii imeingiza Sh milioni 50.9.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic