November 15, 2013





Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, ametamka kuwa kuna mabadiliko yatafanyika katika ngazi ya uongozi katika taasisi hiyo, lakini akakanusha taarifa  kwamba wapo mbioni kumpa ajira aliyekuwa Kocha wa Azam, Stewart Hall, na kusisitza ajira za wengine ikiwemo ya Mkurugenzi wa Ufundi, Sunday Kayuni, bado ipo salama.
 
Malinzi amesema hakuna mazungumzo yoyote kati ya uongozi wake na Stewart kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Kayuni.

“Hatuko katika mazungumzo yoyote na Stewart juu ya kuchukua nafasi ya Ukurugenzi wa Ufundi, nafasi hiyo ina mtu anayeendelea na majukumu yake mpaka hapo tutakapofanya maamuzi mengine.

“Bado kuna watendaji ambao wana mikataba yao, nafikiri tunatakiwa kusubiri, wakati utakapofika tutangaza nafasi zilizo wazi ili kuweza kuruhusu wengine kuomba,” alisema Kayuni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic