November 15, 2013





Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amemtangaza Aggrey Morris wa Azam FC kuwa ndiye nahodha mpya wa kikosi hicho.


Taifa Stars hivi sasa ipo kambini ikijiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya Kenya, Harambee Stars, Jumanne ijayo. Hivyo, Morris atakuwa amechukua nafasi ya Juma Kaseja aliyekuwa nahodha.

Kim alisema cheo hicho ni cha Taifa Stars na siyo cha kikosi cha Kilimanjaro Stars, hivyo badala yake hivi sasa anatafuta mchezaji mwingine atakayempa unahodha kwenye Michuano ya Chalenji itakayofanyika Nairobi, Kenya.

“Cheo hicho atakitumikia akiwa Stars, hivi sasa natafuta nahodha mwingine wa Kilimanjaro maana Aggrey yeye yupo Zanzibar Heroes,” alisema Kim.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic