November 15, 2013





Katika hali isiyokuwa ya kawaida, juzi mashabiki wa soka walitaka kufanya fujo kwenye ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) zilizo chini ya rais mpya, Jamal Malinzi, kisa kikiwa ni kiingilio kikubwa kwenye Uwanja wa Karume uliopo Ilala, Dar es Salaam.


Mashabiki hao walitaka kufanya fujo hizo wakati wa mechi ya kujipima nguvu kati ya Future Taifa Stars dhidi ya Taifa Stars iliyofanyika kwenye uwanja huo ambapo ndipo ofisi za TFF zilipo.

Kiingilio katika mechi hiyo kilikuwa ni Sh 5,000, hali ambayo ililalamikiwa na mashabiki hao waliokuwa wanataka kuingia uwanjani kuishuhudia mechi hiyo, ambapo Malinzi pia alikuwa ni mmoja wa waliohudhuria.

Wengi wa wale waliokuwa wakilalamika, walidai kuwa wamezoea kuingia uwanjani hapo kwa kiingilio cha Sh 500 au 1,000.

“Haya ndiyo ya uongozi mpya ulioshika hatamu sasa, hapa Karume kiingilio kinakuwa elfu tano, usishangae kwenye ligi ikapandishwa na kuwa elfu hamsini,” alihoji shabiki mmoja. Hata hivyo, baada ya vuta-nikuvute ya muda, mashabiki hao walipoa na kuendelea kubaki nje.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic