November 12, 2013



Imani ya kocha wa Al Markhiya kwa kiungo Mtanzania, Mwinyi Kazimoto imezidi kuwa juu.


Kwani Kazimoto ndiye aliyekabidhiwa jukumu la kuichezesha timu hiyo ya daraja la pili nchini Qatar.

Kocha huyo ameamuamini Kazimoto katika mechi zote tisa na amekuwa kiungo tegemeo sasa.

Mtanzania huyo alianza kuonyesha dalili za kuaminiwa na kocha huyo tokea alipotua akitokea Simba.

Akizungumza kutoka Qatar, Kazimoto alisema ligi ni ngumu na ina changamoto nyingi.

“Ni ligi ngumu sana, lakini katika soka ushindani upo. Lakini ninapambana na kwa kuwa kocha kaniamini basi najituma zaidi,” alisema.

Ligi zote nchini humo zimesimama kupisha kikosi chao cha timu ya taifa ambacho kimeingia kambini.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic