November 12, 2013



Wachezaji kadhaa wa Arsenal waliamua kupoza maumivu kwa kwenda kushuhudia mechi ya fainali ya Kombe la Barclays ATP kwenye Uwanja wa Wimbledon jijini London kati ya Novak Djokovic dhidi ya Rafael Nadal.


Djokovic alichukua ubingwa huo kwa kumchapa Nadal bila ya huruma kwa seti mbili za moja kwa moja za 6-3, 6-4.
WILSHERE (KUSHOTO)

ARTETA NA KITU CHAKE

Wakati wakali wakichuana, Jack Wilshere na Mikel Arteta wa Arsenal walikuwa kati ya mashabiki waliojitokeza.

Wawili hao walicheza katika mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Man United ambayo Arsenal ililala kwa bao 1-0, pamoja na kucheza vizuri zaidi.



Hivyo ilionekana wawili hao waliamua kujipoza na kushuhudia mechi hiyo ya wachezaji wakali zaidi duniani iliyoisha kwa Djokovic kuendelea kuonyesha kweli yeye ni namba 1 sahihi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic