November 29, 2013




Kocha mkongwe nchini Abdallah ‘King’ Kibadeni amekubali kutua na kuifundisha Ashanti United ambayo iko katika wakati mgumu.
 
Ashanti iko katika wakati mgumu katika msimamo wa Ligi Kuu Bara na imemaliza mzunguko wa kwanza ikiwa katika nafasi ya 12 kati ya timu 14.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Ashanti zimeeleza, tayari mazungumzo kati ya Kibadeni na kocha huyo yamefanyika, naye ameridhia kutua huko.

“Tayari mazungumzo yamefanyika, naweza kusema ni asilimia 90 tuko katika makubaliano na Kibadeni na amekubali kuja kuifundisha timu yetu. Amesema lile agizo la Rage kumrudisha yeye amelikataa na hatabaki Simba,” kilieleza chanzo.

“Kwa kuwa ametuhakikishia, basi tumeanza kuandaa kila anachotaka na tunasubiri tu amalizane na Simba kuchukua haki yake ili aanze kazi hapa Ashanti.”

Alipotafutwa Kibadeni, jana mchana, alikiri kufanya mazungumzo na Ashanti lakini akasisitiza suala hilo litabaki kuwa siri.

“Kweli siwezi kubaki Simba, huo ni ukweli. Lakini kuhusiana na Ashanti na mambo mengine yote ya Simba nitayazungumza Jumamosi.

“Nimeitisha mkutano na waandishi wa habari, nimewaomba waje kwangu Madale, saa nne kamili asubuhi. Nitaeleza kila kitu kuhusiana na Simba na hata Ashanti, hivyo leo siwezi kuzungumza zaidi,” alisema Kibadeni.

Kibadeni na msaidizi wake, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ walifukuzwa kazi na kamati ya utendaji lakini mwenyekiti aliyesimamishwa, Ismail Aden Rage akawarudisha na kujirudisha madarakani akisema kamati hiyo haikufuata katiba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic