November 29, 2013



Mshambuliaji wa Simba, Amissi Tambwe amesema anatumia muda wake wa mapumziko kuwa bize kusimamia ujenzi wa nyumba yake nchini Burundi katika Mji wa Makamba.


Tambwe alisajiliwa Simba msimu huu akitokea katika kikosi cha Vital O’ ya Burundi. Tayari amefunga mabao 10 kwenye Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na gazeti hili kutoka Burundi, straika huyo alisema: “Nipo bize kusimamia ujenzi wa nyumba yangu kwa sababu ndiyo muda muafaka wa kufanya hivyo kabla sijarejea Tanzania.

“Nyumba hiyo ninayojenga ipo maeneo ya Makamba, lakini hata Bujumbura nina uwanja pia, wasifikiri Simba ndiyo imenijengea ila nina mipango yangu ya muda mrefu ambayo nilikuwa nikiiweka sawa.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic