November 15, 2013





Kocha wa makipa wa Taifa Stars, Juma Pondamali amesema hataki tena kuwa kocha wa makipa na badala yake anataka kuwa kocha mkuu au msaidizi katika ngazi ya klabu.


Pondamali ambaye ni kocha wa makipa wa Coastal Union amesema kuwa kwa sasa kazi hiyo ataifanya akiwa kwenye timu ya taifa pekee hadi hapo baadaye atakapopata ajira anayoitaka.

“Nimeamua kutoendelea kuwa kocha wa makipa tena katika klabu za ligi kuu, ninachohitaji ni kuwa kocha mkuu au msaidizi na siyo zaidi ya hapo, maisha ni mabadiliko na mimi ninahitaji mabadiliko ambayo nimeamua,” alisema kocha huyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic