November 12, 2013



Siku chache baada ya kuibuka ghafla kwenye mazoezi ya mabingwa wa Kenya, Gor Mahia, Kocha Mkuu wa timu ya taifa, Harambee Stars, Adel Amrouche safari hii amekwenda bila taarifa kwenye shule moja jijini Nairobi.


Amrouche raia wa Ubelgiji aliibukia katika shule hiyo bila ya mwaliko na kuwashangaza walimu na wanafunzi waliokuwa wakicheza soka.
AKISHUHUDIA WATOTO HAO..

AKIKARIBISHWA NA KOCHA WA TIMU HIYO YA SHULE

Baada ya hapo alishuhudia mazoezi na baada ya hapo akaungana nao na kuwapa ushauri.

Kocha huyo aliwashauri mambo kadhaa huku akiwapa moyo kwamba kama wakijituma siku moja watakuwa wachezaji wakubwa na maarufu duniani.

AKITOA NASAHA..

Kocha wa timu hiyo alishukuru sana huku akimuambia Amrouche: “Hii ni mara ya kwanza kwa kocha mkubwa kama wewe kuja katika mazoezi yetu, ni kitu kikubwa kwetu na hawa watoto.


“Hata viongozi wetu wamekuwa wakipita tu hapa lakini hakuna hata mmoja ambaye amewahi kuja kutuona.”

SIKU CHACHE ALIPOIBUKA KWENYE MAZOEZI YA GOR MAHIA
AKIMUAGA KOCHA WA GOR MAHIA, BOBBY WILLIAMSON

AKIWA NA MOSES ODHIAMBO

AKIWA NA LAVTSA


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic