November 12, 2013

 
ODHIAMBO AKIWA NA SALEH ALLY KATIKA MAZOEZI YA GOR MAHIA JIJINI NAIROBI
Na Mwandishi Wetu, Nairobi
Pamoja na kuonekana ameshuka kiwango wakati akiwa Yanga, Moses Odhiambo ni kati ya wachezaji walioipa Gor Mahia ubingwa wa Kenya baada ya kuukosa kwa miaka 13.


Odhiambo amekuwa akiendelea kutumika kama mmoja wa wachezaji wakongwe na wenye msaada mkubwa.

Akizungumza na SALEHJEMBE jijini hapa, Odhiambo alisema amekuwa akiendelea kufanya vizuri kwa kuwa anaijua kazi yake.

“Watu wakisema umeshuka wewe ukaamini, basi unakwisha. Lakini mimi sikuamini hilo, nikaendelea kujituma na kufanya mambo yangu.

“Sasa ni kati ya wachezaji ambao tumeweka rekodi ya kuipa Gor ubingwa ilioukosa kwa miaka 13, kitu ambacho kwetu ni kikubwa sana,” alisema Odhiambo aliyewahi kukipa Simba na baadaye Yanga.






0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic