November 14, 2013



Picha inaonyesha wajumbe wawili wa kamati ya usajili ya Yanga, Seif Ahmed ‘Magari’ na Abdallah Bin Kleb lazima kuna jambo.
Hapa walikuwa wanafuatilia mechi ya kirafiki jana, kati ya Taifa Stars dhidi ya Future Taifa Stars kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.


Wawili hawa wanajulikana kwa makali yao kwenye usajili, wakiingia kwenye 18, basi asilimia 95 ni bao na hapa walikuwa kwenye 18.
Tayari wameanza makali yao kwa kumsajili Juma Kaseja ambaye Simba walisema hana kiwango, sasa imeelezwa wanawania kati ya washambuliaji kutoka Ruvu Shooting (Elias Maguri), Mtibwa Sugar (Juma Luizio) au Mbeya City (Mwagano Yeya).


Lakini inawezekana ni danganya toto, kumbe wamemlenga mwingine kabisa. Macho hayo manne huenda yameangalia kwingine. Tusubiri.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic