Na
Mwandishi Wetu
Mashabiki wa Simba na Yanga kwenye
miji ya Tunduma na Morogoro nao watapata fursa ya kuburudika katika michezo
mbalimbali kupitia bonanza maalum la Nani Mtani Jembe lililoandaliwa na Bia ya
Kilimanjaro Premium Lager litakalofanyika uwanja wa Mwaka mjini Tunduma na
Kiwanja cha Ndege mjini Morogoro siku ya Jumapili wikendi hii.
Mratibu wa mabonanza hayo Lawrence
Andrew, amesema kuwa michezo mbalimbali ikiwemo soka bonanza la wachezaji saba
kila upande, kuvuta kamba, na pia mpira wa mezani maarufu kama fussball
itapamba mabonanza hayo. Burudani mbalimbali pia zitapamba bonanza
litakalofanyika Tunduma zikiwemo burudani ya muziki kutoka bendi ya High Class
pamoja na wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya wa mkoani Mbeya.
Kwa Mkoa wa Morogoro bendi maarufu
mkoani humo ya Beacon Sound itatoa burudani kabambe kwa mashabiki
watakaojumuika kushiriki bonanza hilo huku wasanii wa kundi maarufu la dansi
GYT wakilishambulia jukwaa vilivyo.
Andrew pia amesema kuwa vilevile kuwa
michezo mbalimbali ya kujifurahisha kama vile kufukuza kuku wa kienyeji,
kukimbia na gunia na kupiga penati ukiwa umefungwa kitambaa usoni itapamba
mabonanza hayo ambayo yatafanyika katika mikoa hiyo kwa mara ya kwanza kupitia
Nani Mtani Jembe.
Kampeni hii ya aina yake inatoa fursa
ya kipekee kwa mashabiki hao kujumuika pamoja na kuburudika na vile vile
imeongeza chachu ya ushindani na utani wa jadi kati ya mashabiki hao huku
ikiwapa fursa ya kipekee kuonyesha mapenzi kwa timu zao.
Mabonanza hayo yanalotarajiwa kuanza
saa tatu asubuhi ni mwendelezo wa kampeni ya Nani Mtani Jembe ambayo
ilizinduliwa Oktoba 2 na inafanyika nchi nzima ikiwashirikisha
mashabiki wa timu kongwe za Simba na Yanga.
Kupitia kampeni hiyo, Kilimanjaro
Premium Lager inayozidhamini timu za Simba ya Yanga imetenga kiasi cha shilingi
milioni 100 na kisha kuzigawanya kwa timu hizo ambapo kila timu inazo shilingi
milioni 50 ambazo zinashindaniwa na mashabiki wao.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George
Kavishe alisema kuwa mashabikiwa Simba na Yanga wanatakiwa kushindana kwa
kushiriki kwenye kampeni hiyo ili kuhakikisha kuwa timu mojawapo inapata fedha
nyingi zaidi ya timu nyingine.
Akielezea namna ya kushiriki, Kavishe
alisema kuwa mpaka kila timu imetengewa shilingi milioni 50 na kuwa mshiriki wa
shindano hilo la Nani Mtani Jembe ambaye ni shabiki wa Simba au Yanga
anachotakiwa kufanya ni kununua bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo kwenye
kizibo chake kuna namba ya kushiriki.
Alisema baada ya shabiki kununua bia
ya Kilimanjaro na kuona namba ya kwenye kizibo, anachotakiwa kufanya ni
kuchukua simu yake ya kiganjani na kuandika ujumbe mfupi wa maneno akianza na
jina la timu anayoshabikia kisha anaandika namba iliyo kwenye kizibo na kuituma
kwenye namba 15440.
Alisema baada ya shabiki kutuma namba
hiyo, atakuwa amepunguza shilingi 10,000 kutoka kwa timu pinzani yaani ikiwa
shabiki aliyetuma ujumbe huo ni wa Simba atakuwa amefanikiwa kupunguza shilingi
10,000 kutoka kwenye fungu la Yanga na ikiwa shabiki ni wa Yanga pia atakuwa
amepunguza shilingi 10,000 kutoka kwa Simba.
Kwa mujibu wa Kavishe matokeo ya
uwiano wa fedha zinavyopungua kutoka Simba au Yanga yatangazwa kila siku hadi
siku ya mwisho wa shindano hilo Desemba 14, mwaka huu.
Kwa mujibu wa matokeo kama
ilivyotangazwa kwenyehttps://cms.rasello.com/kili tovuti
maalum ya Nani Mtani Jembe timu ya Yanga inaongoza kwa kuwa na kiasi cha
shilingi 55,600,000 huku Simba ikiwa na shilingi 44,400,000 hii ikiwa ni baada
ya Simba kuongoza kwa takribani wiki mbili sasa hatimaye Yanga wamewapita.
0 COMMENTS:
Post a Comment