Na Mwandishi
Wetu
Kampeni ya Kili Nani Mtani Jembe
itaendelea kuunguruma tena Jumapili wiki hii na kuwapa nafasi mashabiki wa
Simba na Yanga walioko Dodoma, Musoma na Singida na kuchuana vikali katika
michezo mbalimbali huku wakihakikisha timu zao zinaibuka na kitita cha shilingi
milioni mia moja zilizotengwa na Kilimanjaro Premium Lager kwa ajili ya Watani
wa Jadi kupitia kampeni hiyo.
Mratibu wa mabonanza hayo, Lawrence
Andrew amesema jijini Dar es salaam jana kwamba mashabiki watapata fursa ya
kushiriki katika michezo mbalimbali kama vile foosball, kuvutana kamba, soka la
wachezaji saba kila upande maarufu kama “Seven aside” na kuongeza kuwa ili
kuhakikisha mashabiki hao wanafurahia ipasavyo burudani mbalimbali za muziki
zitakuwepo pamoja na Nyama choma.
Andrew alisema kuwa katika mji wa mji
wa Dodoma bonanza la Kili Nani Mtani Jembe litafanyika katika uwanja wa shule
ya Dodoma Sekondari ambapo bendi maarufu ya The TNC Band itatumbuiza.
Na huko Musoma bonanza litafanyika katika uwanja wa Mukonde na kupambwa na bendi ya Musoma Stars huku mkoani Singida likifanyika katika Uwanja wa Namfua na burudani kabambe ikishushwa na Wana Pamba Music Band aka Watoto wa Mujini bendi ambayo imejizolea umaarufu mkubwa sana mkoani humo.
Na huko Musoma bonanza litafanyika katika uwanja wa Mukonde na kupambwa na bendi ya Musoma Stars huku mkoani Singida likifanyika katika Uwanja wa Namfua na burudani kabambe ikishushwa na Wana Pamba Music Band aka Watoto wa Mujini bendi ambayo imejizolea umaarufu mkubwa sana mkoani humo.
Andrew pia amesema kuwa vilevile kuwa
michezo mbalimbali ya kujifurahisha kama vile kufukuza kuku wa kienyeji,
kukimbia na gunia na kupiga penati ukiwa umefungwa kitambaa usoni itapamba
mabonanza hayo ambayo yatafanyika katika mikoa hiyo kwa mara ya kwanza kupitia
Nani Mtani Jembe.
Kampeni hii ya aina yake inatoa fursa ya kipekee kwa mashabiki hao kujumuika pamoja na kuburudika na vile vile imeongeza chachu ya ushindani na utani wa jadi kati ya mashabiki hao huku ikiwapa fursa ya kipekee kuonyesha mapenzi kwa timu zao.
Kampeni hii ya aina yake inatoa fursa ya kipekee kwa mashabiki hao kujumuika pamoja na kuburudika na vile vile imeongeza chachu ya ushindani na utani wa jadi kati ya mashabiki hao huku ikiwapa fursa ya kipekee kuonyesha mapenzi kwa timu zao.
Mabonanza hayo yanalotarajiwa kuanza
saa tatu asubuhi ni mwendelezo wa kampeni ya Nani Mtani Jembe ambayo inafanyika
nchi nzima ikiwashirikisha mashabiki wa timu kongwe za Simba na Yanga. Kupitia
kampeni hiyo, Kilimanjaro Premium Lager inayozidhamini timu za Simba ya Yanga
imetenga kiasi cha shilingi milioni 100 na kisha kuzigawanya kwa timu hizo
ambapo kila timu inazo shilingi milioni 50 ambazo zinashindaniwa na mashabiki
wao.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George
Kavishe alisema kuwa mashabikiwa Simba na Yanga wanatakiwa kushindana kwa
kushiriki kwenye kampeni hiyo ili kuhakikisha kuwa timu mojawapo inapata fedha
nyingi zaidi ya timu nyingine.
Akielezea namna ya kushiriki, Kavishe
alisema kuwa mpaka kila timu imetengewa shilingi milioni 50 na kuwa mshiriki wa
shindano hilo la Nani Mtani Jembe ambaye ni shabiki wa Simba au Yanga
anachotakiwa kufanya ni kununua bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo kwenye
kizibo chake kuna namba ya kushiriki.
Alisema baada ya shabiki kununua bia ya
Kilimanjaro na kuona namba ya kwenye kizibo, anachotakiwa kufanya ni kuchukua
simu yake ya kiganjani na kuandika ujumbe mfupi wa maneno akianza na jina la
timu anayoshabikia kisha anaandika namba iliyo kwenye kizibo na kuituma kwenye
namba 15440.
Alisema baada ya shabiki kutuma namba
hiyo, atakuwa amepunguza shilingi 10,000 kutoka kwa timu pinzani yaani ikiwa
shabiki aliyetuma ujumbe huo ni wa Simba atakuwa amefanikiwa kupunguza shilingi
10,000 kutoka kwenye fungu la Yanga na ikiwa shabiki ni wa Yanga pia atakuwa
amepunguza shilingi 10,000 kutoka kwa Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment