November 21, 2013



PICHA ALIYOPIGA INIESTA


Kiungo nyota wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, Iniesta ameonyesha furaha kurejea na kuliona live goli alilofunga bao siku ya mwisho ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010.


Iniesta alipiga picha za lango hilo ambalo liko kwenye Uwanja wa Soccer City, Johannesburg, Afrika Kusini.

“Nimefurahi kurudi hapa,” aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter.

Iniesta na kikosi cha Hispania ambao ni mabingwa Dunia walikuwa nchini humo kucheza mechi ya kirafiki waliyolala kwa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Bafana Bafana.

Katika michuano hiyo mwaka 2010, Hispania ilishinda bao 1-0 katika fainali na kubeba kombe hilo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic