November 15, 2013



Mshambuliaji mkongwe, Gaudence Mwaikimba na beki wa pembeni, Malika Ndeule, wametangazwa kuwa huru baada ya kumalizana na Azam FC.


Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa wachezaji hao wamemalizana na klabu hiyo, kuhusu kuendelea kubaki klabuni hapo itategemea na ujio wa kocha mpya atakayefika hivi karibuni kuchukua nafasi ya Stewart Hall.

“Mwaikimba na Ndeule ndiyo wachezaji pekee ambao mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwanzoni mwa Desemba, mwaka huu, hivyo wapo huru kufanya mazungumzo na klabu yoyote itakayowahitaji.

“Lakini sidhani kama watabaki, mfano Mwaikimba ni mchezaji mzuri lakini umri nao umeenda sana, lakini kama akipata timu nyingine bado anao uwezo wa kucheza katika ligi kuu,” kilisema chanzo hicho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic