November 14, 2013

HASHEEM KATIKA MOJA YA MECHI ZA NBA

Timu ya Oklahoma City Thunder anayoitumikia Mtanzania Hasheem Thabeet imepoteza mchezo wake wa ugenini dhidi ya Los Angeles Clippers.


Clippers walifanikiwa kushinda kwa pointi 111-103 za wageni hao ambao walionekana kama wangeshinda huku mshambuliaji wao, Kelvin Durant akionekana kuwa msumbufu zaidi.

Katika mechi hiyo ya NBA iliyochezwa jana jijini Los Angeles, wenyeji walikuwa nyuma katika vipindi vyote viwili hadi mapumziko.

Lakini wakacharuka katika vipindi viwili vya mwisho na kufanikiwa kusawazisha kabla ya kutangulia na baadaye kuibuka na ushindi.

Thabeet ambaye ni Mtanzania na pekee kutokea Afrika Mashariki anayecheza katika ligi hiyo maarufu alicheza kwa zaidi ya dakika 15 katika mchezo huo.



103

111

FINAL

OKC
LAC
33291625103
25283028111

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic