November 14, 2013


Mshambuliaji nyota wa Simba, Amissi Tambwe amesema bado ana kazi ya kufanya na Simba.


Tambwe raia wa Burundi amesema angependa kubaki Simba na kuendelea kufanya kazi.

“Lakini kama kutakuwa na makubaliano kati ya Simba na klabu nyingine, pia ninaweza kwenda.

“Lakini napenda kucheza ligi ya Tanzania angalau msimu mmoja nikiwa pale na Simba,” alisema.

Hata hivyo, Tambwe hakutaka kuzungumzia zaidi kuhusiana na Simba, hali iliyoonyesha huenda kuna tatizo.
“Sasa kidogo kuhusu Simba nisingependa kuzungumza zaidi ya hapa,” alisema.
Kumekuwa na taarifa timu kadhaa zimeonyesha nia ya kumchukua Mrundi huyo anayeongoza kwa kupiga mabao ligi kuu, ana bao 10.
Hata hivyo, tayari uongozi wa Simba umeishasema hauna mpango wa kumuuza na kuwataka wanaomuania waachane na wazo hilo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic