Na Boniface Wambura wa TFF
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeandaa mechi mbili za majaribio ya matumizi ya tiketi za
elektroniki zitakazochezwa Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam.
Mechi
ya kwanza itakuwa Desemba 26 mwaka huu saa 10 jioni ambapo itazikutanisha timu
za Azam na Ruvu Shooting. Mechi nyingine itachezwa Januari Mosi mwakani kwa
kuzikutanisha Ashanti United na JKT Ruvu.
TFF
tunatoa mwito kwa washabiki kujitokeza katika mechi hizo ambapo mbali ya
kushuhudia burudani pia watajionea jinsi mfumo huo wa tiketi za elektroniki
unavyofanya kazi.
Kwa
kushirikiana na benki ya CRDB ambayo ndiyo iliyoshinda tenda hiyo ya tiketi za
elektroniki, TFF imepanga vilevile kuandaa mechi nyingine majaribio mikoani
kabla ya mfumo huanza kutumika rasmi Januari 25 mwakani katika mzunguko
wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).
0 COMMENTS:
Post a Comment