December 20, 2013

OKWI MAZOEZINI NA YANGA LEO ASUBUHI


 
Baada ya hadithi nyingi za Mwenyekiti wa Simba aliyesimamishwa, Ismail Aden Rage, Okwi ameweka tayari rekodi mbili na Yanga.
 
Moja ilikuwa jana alipovaa kwa mara ya kwanza jezi ya Yanga na kupokelewa na viongozi wa timu hiyo.
Lakini leo, ameweka nyingine baada ya kufanya mazoezi na timu hiyo akiwa chini ya Kocha Mholanzi, Ernie Brandts.

Katika mazoezi hayo kwenye Uwanja wa Bora Kijitonyama jijini Dar, Okwi alikuwa kivutioo kikubwa na watu wengi walijitokeza kumshuhudia.
Rage amekuwa akisisitiza Okwi hatocheza Yanga, huenda kesho kauli yake hiyo ikafutika kabisa atakapoichezea Yanga katika mechi ya Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba.

Baada ya mechi hiyo, kitakachosubiriwa ni Okwi kucheza mechi ya mashindano, suala ambalo Rage atakuwa amepoteza cha kusema.

Rage ameendelea kusisitiza kwamba Okwi hatakiwi kucheza Simba, lakini Yanga wanaendelea na mambo yao kama kawaida.

















0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic