December 11, 2013





Beki mpya wa Saraswot Youth Club ya Nepal, Shadrack Nsajigwa, anaendelea na mazoezi ya timu hiyo huku akilalamikia baridi kali inamsumbua.


Nsajigwa na wenzake Pius Kisambale na Godfrey Bonny ‘Ndanje’, walitimkia nchini humo kwa ajili ya kwenda kucheza soka la kulipwa.

Nsajigwa amesema kikwazo kwake nchini huko ni baridi pekee ambayo ameahidi kupambana nayo.

Nsajigwa alisema tayari ameanza mazoezi na timu hiyo wakijiandaa na ligi kuu ya nchini humo inayotarajiwa kuanza wiki mbili zijazo.

“Huku ninaendelea vizuri, kikwazo kwangu huku ni hali ya hewa ya baridi ambayo ni kali sana, lakini haitanizuia kuendelea kubaki kupambana katika kutafuta maisha.

“Tumeanza mazoezi ya pamoja na wachezaji wenzetu kujiandaa na ligi kuu, itakayoanza wiki mbili zijazo,” alisema Nsajigwa aliyewahi kuwa nahodha wa Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic