December 11, 2013





Hali ya kiafya ya aliyekuwa kocha wa makipa wa Simba, James Kisaka, bado siyo nzuri, baada ya kubadilika ghafla.


Kisaka anayesumbuliwa na matatizo ya kutetemeka kwa miguu na kuvimba kwa jicho lake la kulia, hali yake imebadilika ambapo sasa miguu yake imepungua nguvu na kumpa tabu zaidi katika kutembea.

Championi Jumatano lilimtembelea Kisaka ambaye ni kipa wa zamani wa Simba na kumkuta nyumbani kwa kaka yake Msasani jijini Dar, akiwa hoi huku akiongea kwa tabu ambapo amesema maumivu ya kichwa yanazidi kuongezeka.

Amesema alikuwa akitumia tiba ya kutundikiwa maji ‘drip’ ambayo tayari ameshamaliza na sasa anaendelea kutumia vidonge mbalimbali alivyoandikiwa katika hospitali mbalimbali, ambavyo vimeshindwa kubadilisha hali yake.

“Hali yangu siyo nzuri, imebadilika kidogo, juzi ulivyokuja (wiki iliyopita) nilikuwa naweza kutembea kidogo ingawa kwa kusaidiwa lakini sasa miguu yangu yote imezidi kupungua nguvu na kunipa tabu katika kutembea, naumwa kwa kweli,” alisema Kisaka kwa uchungu.

“Nilikuwa natumia drip ambazo sasa zimeshakwisha, naendelea kutumia vile vidonge nilivyoandikiwa, lakini sasa maumivu ya kichwa nayo yanazidi katika siku mbili hizi, hapa nazungumza na wewe kwa sababu nakuheshimu sana lakini ingekuwa mtu mwingine ningemuomba aniache,” alisema Kisaka kwa shida.
 SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic