December 23, 2013




Hali ya winga nyota wa zamani wa Yanga na Simba, Edibily Lunyamila imeimarika kwa jioni hii.


Lunyamila amelazwa katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo.

Taarifa zilizotufikia punde, Lunyamila anaendelea vizuri ukilinganisha na mchana.

Mashine za msaada wa kupumua zimeondolewa na sasa anaweza kupumua mwenyewe.

Ndugu yake wa karibu amesema kuna nafuu ingawa bado hali yake haijaiamarika sana.
“Bado haijawa nzuri sana lakini sasa ni afadhari,” alisema.
Lunyamila ambaye sasa ni mchambuzi wa masuala ya soka katika gazeti la CHAMPIONI ameanza kusumbuliwa na presha hivi karibuni.
Mwanasoka huyo aliyechipukia kisoka mkoani Shinyanga ingawa ni mwenyeji wa Kigoma alikuwa akisifika kwa kasi na mashuti makali wakati anakimbia na mpira lakini krosi za maana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic