December 23, 2013

KASEJA AKITOKA UWANJANI BAADA YA MECHI DHIDI YA SIMBA

Kipa mpya wa Yanga, Juma Kaseja, amewaomba msamaha mashabiki wa timu hiyo baada ya kuruhusu mabao matatu kuingia wavuni katika mechi ya Nani Mtani Jembe iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Hii ilikuwa mechi ya kwanza kwa Kaseja kucheza tangu atue kujiunga na timu hiyo kwenye usajili wa dirisha dogo lililofungwa Desemba 15, mwaka huu akitokea Simba baada ya mkataba wake kumalizika.

Tukio hilo la kuwaomba msahamaha mashabiki wa Yanga, kipa huyo alilifanya mara baada ya mechi kumalizika, akitoka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kuelekea kwenye basi la timu hiyo.


Wakati anaelekea kwenye basi hilo, kundi kubwa la mashabiki wa timu hiyo lilimvamia Kaseja aliyekuwa amezungukwa na makomandoo wa Yanga na kuhoji sababu za kufungwa mabao hayo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic