December 23, 2013

TAMBWE AKISHANGILIA BAADA YA KUIFUNGIA SIMBA BAO LA KWANZA

Bao la kwanza la mshambuliaji wa kimataifa wa Simba, Amissi Tambwe, lilisababisha askari wa usalama barabarani ‘traffic’ aliyekuwa na sare za kazi, kushangilia na kuvunja kiti Uwanja wa Taifa, Dar kutokana na furaha iliyozidi.


Juzi, Simba na Yanga zilicheza mchezo wa Nani Mtani Jembe, Simba ikashinda mabao 3-1, lakini kuhusu shindano la vinywaji lililohusu mashabiki, Yanga ilijinyakulia Sh milioni 98.4 wakati Simba ikipata Sh milioni 1.6, kati ya Sh milioni 100 zilizokuwa zikigombewa.

Baada ya Tambwe ambaye alipachika mabao mawili, kufunga bao la kwanza, traffic huyo ambaye hakuweza kufahamika jina, alipagawa na kusababisha kuvunja kiti alipokuwa akishangilia katika jukwaa la Simba.

Tambwe alifanikiwa kupachika bao la kwanza dakika ya 13.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic