Imefahamika kiungo mkongwe, Per
Mertesacker alijikuta akimshambulia kwa maneno rafiki yake Mesut Ozil baada ya
kuwaonyesha pozi mashabiki wa Arsenal.
Mara baada ya Arsenal kupokea kipigo
cha mabao 6-3 kutoka kwa Man City, Mertesacker na Ozil walizozana wakati wakitoka uwanjani.
Baadaye ilielezwa hali hiyo ilitokana
na Mertesacker kumlaumu Ozil kushindwa
kuwashukuru mashabiki wa Arsenal waliosafiri kutoka London hadi Manchester
katika mechi hiyo.
Ozil hakuonyesha kujali na alimjibu
maneno yaliyoonyesha kumuudhi Mertesacker ambaye alimfuata akionekana kuwa na hasira
zaidi.
Baadaye Mertesacker alirusha shati yake kwa mashabiki hao
kuonyesha heshima kwao na kuthamini sapoti yao.
Kuhusiana na hilo, Wenger alisema: “Wajerumani
wanajuana na usiwe na wasi, watalimaliza wenyewe.”
Mertesacker na Ozil wote ni wachezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani, halafu washkaji kinoma.










0 COMMENTS:
Post a Comment