December 25, 2013





Kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi, amesema yupo tayari kuifundisha Yanga kama kocha msaidizi iwapo atahakikishiwa maslahi mazuri.

Mwambusi ambaye amefanikiwa kuipandisha Mbeya City msimu huu na kucheza Ligi Kuu Bara amekuwa akiwindwa na Yanga kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Fred Felix Minziro.


 Mwambusi amesema taarifa hizo hajazipata rasmi kutoka kwa viongozi wa mabingwa hao watetezi wa ligi kuu lakini iwapo watamfuata atawasilikiza na kuwatajia dau ambalo yeye anataka.
Alisema yeye kama kocha, kazi yake ni kufundisha mpira, hivyo yupo tayari kwenda popote iwapo tu atapata maslahi mazuri.
“Taarifa rasmi sijazipata lakini wakinifuata nitaongea nao kwa kuwa tayari watakuwa wameonyesha kuniheshimu kutokana na kazi ninayoifanya kukubalika kwao,” alisema Mwambusi. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic