December 25, 2013





Kiungo wa Azam, Mcha Khamis 'Vialli', atakuwa nje ya dimba kwa wiki moja akiuguza goti lake la kushoto aliloumia akiwa kwenye kikosi cha timu ya taifa katika michuano ya Chalenji.


Daktari wa Azam, Mwanandi Mwankemwa, alisema tayari kiungo huyo baada ya kutibiwa ameanza mazoezi mepesi na atajiunga na wenzake baada ya wiki moja.
Alisema wachezaji wengine wote wapo fiti wakijiandaa na Michuano ya Mapinduzi inayotarajiwa kufanyika Januari mwakani mjini Zanzibar.
“Wachezaji wote wapo vizuri isipokuwa Mcha ambaye ana tatizo la goti la kushoto aliloumia kwenye Michuano ya Chalenji, nimempa wiki moja zaidi ili ajiunge kwenye mazoezi na wenzake,” alisema Mwankemwa ambaye pia ni daktari wa timu ya taifa (Taifa Stars).

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic