December 21, 2013



MPIRA UMEKWISHAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
Dk 90+2 Yanga wanafanya shambulizi lakini pasi ya mwisho ya Domayo inakuwa fupi na Ivo anafanya Mbwembwe

 
Dk 90+1 Simba wanaonekana kupoteza muda zaidi
Dk 90, Yanga wanafanya shambulizi lakini Tegete anashindwa kumalizia kwa kuwa mpira mrefu zaidi
GOOOOOOO Dk 87 Okwi anaifungia Yanga bao kwa kichwa baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Simba na kuunganisha krosi nzuri ya Msuva


Dk 84 Simba wanamtoa Redondo anaingia Humud
Dk 81 Yondani anapewa kadi ya pili ya njano, inakuwa nyekundu..NJE, alimuangusha Messi baada ya kumyanyasa
Dk 79 Yanga wanamtoa Luhende anaingia Oscar Joshua


Dk 76 Okwi anawatoka mabeki wa Simba na kupiga shuti linatoka nje
Dk 73, Simba wanamtoa Badru anaingia Zahor Pazi
Dk 70, Yanga wanamtoa Ngassa anaingia Tegete


Dk 64, Ivo anautema mpira, unakwenda kwa Okwi ambaye anapiga shuti linagonga mwamba na kutoka nje


GOOOOOOOOOO Dk 62, Badru anafunga bao baada ya kosa la Juma Kaseja aliyetaka kuurudisha mpira eneo la hatari, akaanguka na mfungaji akauwahi 
Dk 61 Simba wanafanya shambulizi kubwa zaidi tokea kuanza kwa mechi, Kaseja anaokoa, krosi ya Uhuru mpira wa Messi unagonga mwamba wa juuu.
Dk 58 Simba wanafanya mabadiliko tena anatoka Tambwe anaingia Amri Kiemba
Dk 56, Simba wanamtoa Chanongo na nafasi yake inachukuliwa na Uhuru Selemani 


Dk 54, Yanga wanamtoa Cannavaro anaingia Juma Abdul
Dk 51, Cannavaro anaunganisha kichwa safi lakini mpira unatoka nje kidogo
Yanga imewatoa Kavumbagu, Kiiza na Chuji, nafasi zao zimechukuliwa na Okwi, Simon Msuva na Hassan Dilunga
 Kipindi cha pili kimeanza


half time
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
GOOOO...dk 43 Tambwe anakwenda, gooooooooooooooooooooo
PENAAAAAT..dk 42, Luhende anamuangusha Messi ndani ya 18, hadi sasa anapata matibabu.




Dk 36 Simba wanafanya mashabulizi na pasi huku Yanga wakionekana kupoteza mwelekeo
Dk 35, Mkude anapiga bonge la shuti ndani ya mita 31 lakini linatoka nje kidogo 


Dk 34 Kaseja anafanya kazi ya ziada kuokoa shuti la Badru
Dk 31, Simba wanamtoa Henry Joseph anaingia Ramadhani Chombo
Dk 26 Simba inafanya mabadiliko anatoka Said Ndemla anaingia Ramadhani Singano 'MEssi'
 Dk 24 Tambwe anapiga kichwa kwa mpira wa krosi wa Henry uunatoka sentimeta chache.
 Dk 17, Simba wanajibunshambulizi kali lakini Chanongo akiwa na Kaseja anashindwa kufunga na kupiga shuti kuubwaaa
 Dk 16, Yanga wanafanya shambulizi kali na Ivo Mapunda anafanya kaziya ziada na kuokoa.
  GOOOOO DK 13, Amissi Tambwe anapiga shuti la chini baada ya pasi ya Chanongo aliyegongeana na Henry Joseph na kuandika bao la kwanza kwa Simba.
Dk 6, Yanga wanafanya shambulizi tena lakini Ngassa anakuwa si makini.
Dk 2, Yanga wanafanya shambulizi na Cannavaro anapiga shuti kuubwa nje.






0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic