Mwenyekiti wa Simba aliyesimamishwa,
Ismail Aden Rage, amepingwa kwa mara nyingine na wajumbe wa kamati ya utendaji
ya timu hiyo, kufuatia maamuzi ya kuwateua Michael Wambura na Rahma Al Kharusi,
maarufu kama Malkia wa Nyuki.
Swedi
Nkwabi ambaye ni Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba, alisema Rage katika kuwateua
Wambura na Malkia wa Nyuki ni hatua nyingine ya kiongozi huyo kuvunja katiba ya
klabu hiyo.
“Katiba ibara ya 28 kipengele D,
inatamka wazi kuwa mwenyekiti amepewa nafasi ya kuteua wajumbe wawili, ambao
kati ya hao tayari Rage alishamteua Zacharia Hans Pope kuwa mjumbe wa heshima,
huku akibakiza nafasi moja ambayo bado haijakamilishwa vigezo vyake.
“Siku zote tunasema Rage anavunja katiba, watu
huwa hawatuelewi,” alisema Nkwabi huku akiongeza kwa kusema:
“Nafasi moja iliyosalia Rage kama
angekuwa madarakani, angeweza kuitumia lakini ni mpaka pale ambapo angeunda
kwanza baraza la wazee ambalo wakati
tunamsimamisha hakuwa ameliunda.
“Baraza la wazee linaundwa na wajumbe
wanne wa wadhamini wa klabu, wajumbe wanne kutoka baraza la walezi wa klabu na
wajumbe watano ambao hawa wanachaguliwa katika kikao cha wadhamini na walezi,
kikao ambacho mpaka tunamsimamisha alikuwa hajakifanya.
“Lakini pia angalia amemteua Malkia wa
Nyuki kuwa mjumbe wa baraza la wadhamini wakati tayari kolamu yao imeshatimia
baada ya kumteua Patel (Ramesh), Mzee Kilomoni (Hamis), Samuel Sitta na Aluu Habu
ambapo sasa kama amemteua na Malkia wa Nyuki watakuwa watano.”
Aidha, Nkwabi amesema kamati yake haina
tatizo na Wambura au Malkia wa Nyuki ambao wote bado michango yao inahitajika
ndani ya Simba lakini tatizo kubwa lipo kwa Rage ambaye amewaingiza bila
kufuata taratibu.
0 COMMENTS:
Post a Comment