Kocha Mkuu wa Azam FC, Joseph Omog, juzi
na jana alianza kazi kwa kukutana na viongozi wa benchi la ufundi la timu hiyo
na kuwaona baadhi ya wachezaji, lakini akashindwa kufundisha, sababu kubwa
ikiwa ni Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Said Morad na wachezaji wengine ambao
hawapo na timu hiyo.
Omog
amesema amewaona baadhi ya wachezaji wa timu hiyo na ameridhishwa na viwango
vyao, ikiwa ni pamoja na kufanya kikao na benchi lake la ufundi, lakini hataweza
kuanza kufundisha rasmi mpaka nyota wote watakapokamilika.
Omog, raia wa Cameroon, amesema anataka
kuanza kazi baada ya nyota wote kukamilika, ambapo atawasubiri nyota waliopo
katika Michuano ya Kombe la Chalenji; Sure Boy, Morad, Aishi Manula, Farid
Mussa, Erasto Nyoni, Ismail Gambo, Himid Mao na Joseph Kimwaga waliopo katika
kikosi cha Kilimanjaro Stars pamoja na Khamis Mcha na Waziri Salum ambao wapo
na Zanzibar Heroes.
“Nimewaona wachezaji wakifanya mazoezi
lakini walikuwa ni baadhi tu, lakini pia nimekutana na benchi la ufundi
tukazungumza kidogo, tumetambuana lakini sikufanya lolote katika kufundisha leo
(juzi),” alisema Omog, beki wa zamani wa Cameroon huku akiongeza kwa kusema:
“Bado wachezaji wote hawajakamilika, ni
vyema nikakutana na wachezaji wote kwanza na baada ya hapo ndipo tukaanza kazi
yetu rasmi, hawa waliopo katika michuano ndiyo watakaotuzuia kuanza mapema
lakini nafikiri mpaka wiki ijayo tunaweza kuanza.”
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment