December 23, 2013


Kocha Ernie Brandts rasmi ameachishwa kazi ya kuinoa Yanga.

Kocha huyo raia wa Uholanzi amepewa siku 30 ili awe ameondoka zake.
Lakini kwa kawaida ndiyo hatafanya kazi Yanga kwa kuwa timu hiyo ina mambo mengi ya kufanya na haiwezi kusubiri.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Abdallah Bin Kleb amewaambia waandishi leo makao makuu ya klabu hiyo jijini Dar kwamba watamlipa Brandts kila kitu chake.
Gazeti la michezo la Championi ndiyo lilikuwa la kwanza kuandika kuhusiana na taarifa hiyo leo asubuhi.

Brandts ameondoka Yanga baada ya kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Yanga katika mechi ya Nani Mtani Jembe juzi Jumamosi.

1 COMMENTS:

  1. Hapo jana mwenyekiti wa club ya yanga alitangaza kwamba mechi ya nani mtani jembe ilikuwa ni bonanza lkn Hatimae bonanza lamfukuza kocha jangwani

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic