January 19, 2014

MANJI AKIFUNGUKA

Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji leo amemtolea uvivu mzee maarufu wa klabu hiyo, Ibrahim Akilimali na kumtaka aache kuzungumza hovyo kama vile kiongozi.


Manji amemueleza mzee Akilimali mbele ya wanachama zaidi ya 400 waliojitokeza kwenye mkutano wa wanachama uliofanyika kwenye Ukumbi wa PTA jijini Dar es Salaam.
MZEE AKILIMALI AKIMSIKILIZA MANJI


Huku wengi wakiwa hawatarajii, Manji alimtaka mzee Akilimali kufuata katiba na kuachana na kuzungumza mambo ilimradi.

“Mambo yamekuwa ni mengi, si sahihi kuzungumza kila kitu, nakuheshimu sana na wewe ni mzee wangu.
“Lakini si sahihi kuzungumza tu bila ya ruhusa ya uongozi, msemaji wa klabu ni mwenyekiti na kuna viongozi.

“Nimesema ninakuheshimu, nimekukuta Yanga, umenipokea na kuniunga mkono na ndiyo maana leo niko hapa.
“Lakini nakueleza ukweli na ninaamini kwa kuwa nimefanya utaelewa na kujirekebisha,” alisema Manji huku wanachama wakimshangilia.
WAKIKUMBATIANA

Baada ya hapo, Manji alikwenda kuzungumza na mzee Akilimali, wakapeana mikono na kukumbatiana.
Baadaye Manji aliendelea na masuala mbalimbali ikiwemo kuzungumzia mwenendo wa Yanga katika michuano mbalimbali.

Pamoja na hivyo, Manji alihimiza suala la nidhamu kwa wanachama huku akisisitiza watakaokiuka, basi atawatimua mara moja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic