January 20, 2014


MESSI  (KULIA) AKIWA KAZINI

Washambuliaji Amissi Tambwe, Ramadhan Singano ‘Messi’ na Haruna Chanongo, leo Jumatatu wanatarajiwa kuanza mazoezi mepesi baada ya kutoka kwenye majeraha.
Wachezaji hao juzi Jumamosi walishindwa kucheza kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Mtibwa kutokana na kusumbuliwa na majeraha. Simba ilifungwa 1-0 katika mchezo huo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.


Daktari wa Simba, Yassin Gembe, alisema Tambwe alikuwa akisumbuliwa na nyama za paja alizoumia mazoezini, Messi aliumia kidole gumba cha mkono kwenye mechi ya fainali ya Kombe la Mapinduzi wakati Chanongo aliteguka kiganja cha mkono.
Alisema nyota hao leo Jumatatu watakuwa na programu ya kufanya mazoezi mepesi kwenye Uwanja wa Kinesi, Shekilango jijini Dar.

“Nina majeruhi watatu ambao ni Tambwe, Singano na Chanongo, lakini wote wataanza mazoezi mepesi kesho (leo) tayari kwa maandalizi ya mzunguko wa pili,” alisema Gembe.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic