Katika hali isiyo ya kawaida kipa wa
Yanga, Juma Kaseja, jana Alhamisi alijaza mashabiki wa timu hiyo katika Uwanja
wa Bora Kijitonyama alipokuwa akifanya mazoezi binafsi bila kuwa na wenzake
ambao hawakuwepo.
SALEHJEMBE ilishuhudia
mashabiki wengi wakikusanyika uwanjani hapo kuangalia mazoezi ya Yanga lakini
wakamkuta Kaseja, ambapo alikuwa akifanya mazoezi huku akisaidiwa na rafiki
zake waliokuwa wakimrushia mipira.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Kaseja
alisema kuwa alikuwa akifanya mazoezi binafsi kwa kuwa wenzake wapo kwenye
mapumziko.
“Nilikuwa na taarifa kabisa kuwa timu
haitakuwa na mazoezi kwa sababu tuna kikao klabuni cha wachezaji na viongozi
ndiyo maana nikaamua kuja kufanya mazoezi yangu binafsi.
“Kuna rafiki yangu anaishi hapa karibu
ndiye nimekuja naye kunifanyisha mazoezi hapa uwanjani kwa sababu siku nyingine
huwa naenda ufukweni,” alisema Kaseja ambaye wakati anaondoka uwanjani hapo
alilazimika kuruka geti kwa kuona akizunguka atachelewa.
0 COMMENTS:
Post a Comment