Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atakuwa mgeni rasmi
katika ufungaji wa semina ya waamuzi na makamisha leo (Januari 4 mwaka huu) saa
4 asubuhi kwenye ukumbi wa mikutano Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Waamuzi
zaidi ya 100 na makamishna 50 wameshiriki katika semina hiyo. Makamishna hao ni
baadhi ya wale wanaosimamia mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja
la Kwanza (FDL) wakati waamuzi ni wale wa daraja la kwanza (class one) ambao
ndiyo wanaochezesha mechi za VPL na FDL.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatarajia kuandaa semina nyingine baadaye
mwaka huu kwa makamishna wapya wanaotaka kusimamia mechi za VPL na zile za FDL.
0 COMMENTS:
Post a Comment